Hizi kodi mnataka tukaishi kwenye nyumba za udongo?- Mh. Salome


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamependekeza Serikali kupunguza kodi kwenye vifaa vya kodi vinavyotumika kwa ujenzi ya makazi ya wananchi ili kuwaondolea mzigo wananchi.

Akichangia hotuba ya bajeti ya 2023/2024 Mbunge wa Viti Maalum Mh. Salome Makamba amesema kwamba, vifaa vinavyotumika kwa ujenzi wa makazi vinajulikana viwekwe alama ili viuzwe kwa bei nafuu kwa wananchi.

“Serikali mwaka jana iliongeza kodi kwenye nondo na mabati, mwaka huu kwenye sementi, hivi mnataka tukaishi kwenye nyumba za udongo?” alihoji Mh. Salome.

Amesema anaelewa lengo la Serikali kwa kuwa sekta inayozalisha sementi, nondo/chuma na mabati inabiashara kubwa sana, lakini wasisahauliwe Watanzania wa kawaida ambao wanatumia bidhaa hizo kujiboreshea maisha.

“Serikali inamifumo yake ambayo inaweza kujua manunuzi haya yanafanyika kwa ajili ya viwanda, miundombinu na manunuzi haya yanafanyika kwa ajili ya wananchi kujiboreshea mazingira yao ya kuishi,” alisema Mh. Salome.

Chapisha Maoni

0 Maoni