Chelsea yaitolea nje ofa ya pili ya Manchester United

 

Ombi la pili la Manchester United la dau la paundi milioni 50 ili kumnasa kiungo wa Chelsea Mason Mount, limekataliwa.

Mount, 24, anawaniwa na Meneja wa United Erik ten Hag, katika kuimarisha kikosi chake baada ya kufuzu kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Chelsea iliyotumia paundi milioni 600 msimu uliopita, inapaswa kuwauza wachezaji wake kabla ya Juni 30, ili kukidhi matakwa ya Financial Fair Play.

Timu ya Chelsea inajua kuwa thamani ya Mount inafikia kiasi cha paundi milioni 70.

Chapisha Maoni

0 Maoni