Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu wa Alsalam Internatinal Hospital
ya nchini Misri, imefanya kambi ya upasuaji wa kupitia matundu madogo
(Laparoscopy surgery) kwa muda wa siku mbili ambapo kina mama watano
wamenufaika na matibabu hayo.
Akizungumza
wakati wa kufunga kambi hiyo leo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na
Upasuaji wa Matundu Madogo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Vincent Tarimo
amesema waliofanyiwa upasuaji huo wengi walikuwa na changamoto ya uvimbe kwenye
kizazi.
“Upasuaji wa
matundu madogo hufanyika kwa kutoboa sehemu ndogo ya mwili kwa kuingiza vifaa
maalumu ambapo una faida nyingi kwa kuwa mgonjwa hapati majeraha makubwa na
uvujaji wa damu hivyo kupona haraka ili kuendelea na shughuli zake baada ya
muda mfupi,” amesema Dkt. Tarimo.
#Muhimbilitaifa
#MuhimbiliMloganzila
0 Maoni