Madonna alazwa ICU akisumbuliwa na bakteria

Madonna amehairisha ziara yake ya dunia, baada ya kupelekwa hospitali na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), akisumbuliwa na maambukizi makali ya bakteria.

Kwa mujibu wa meneja wake, maambukizi yaliyompata nyota huyo wa muziki wa pop ni hatari, na anapaswa kukaa siku kadhaa katika chumba cha ICU.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Guy Oseary, imesema kwamba afya ya Madonna inaimarika, lakini bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari.

Madonna mwenye umri wa miaka 64, alikuwa anatarajiwa kuzindua ziara yake ya muziki iitwayo 84-date tour, mwezi ujao.

Chapisha Maoni

0 Maoni