Arsenal kumsajili Rice kwa paundi milioni 105

 

Timu ya Arsenal imekubali kumsajili mchezaji kiungo wa West Ham, Declan Rice, kwa dau la paundi milioni 105.

Mazungumzo yanaendelea baina ya klabu hizo mbili, kuhusu namna makubaliano yao hayo yatakavyotekelezwa.

Hii ni baada ya Arsenal kutoa ofa ya tatu, baada ya ofa zao mbili za mwanzo kukataliwa kwa kutoa dau la chini ya paundi milioni 100.

Awali, Manchester City, ambao walitoa ofa ya paundi milioni 90 iliyokataliwa Jumanne, walijiondoa kwenye mbio za kunasa saini ya Rice.

Chapisha Maoni

0 Maoni