Ufaransa kwachafuka magari yachomwa moto

 

Watu 150 wamekamatwa maeneo mbalimbali nchini Ufaransa, kufuatia ghasia zilizotokana na polisi kumpiga risasi na kumuua dereva kijana wa miaka 17.

Kijana huyo Mfaransa mwenye asili ya Algeria, Nahel M, alipigwa risasi kwa karibu baada ya kukataa kusimamishwa na trafiki na kuamuaondoka.

Katika eneo la Nanterre, ambapo Nahel alipigwa risasi, magari yamechomwa moto na polisi walifyatua mabomu ya machozi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliitisha mkutano wa dharura na kusema ghasia hizo hazipaswi kuhalalishwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni