Jela ‘yamuita’ mtoto wa kiume wa Rais Joe Biden

 

Mtoto wa Rais wa Marekani Joe Biden, Hunter Biden anatarajiwa kukiri makosa mawili, katika kujaribu kuepuka kifungo cha jela.

Hunter anakabiliwa na makosa ya kukwepa kodi, pamoja na kukiri kumiliki silaha akiwa anatumia madawa ya kulevya, baada ya uchunguzi wa miaka 5.

Mwanasheria amewasilisha nyaraka zinazoashiria makubaliano ya kukiri makosa na anatarajiwa kukubali matibabu ya kuachana na dawa za kulevya.

Kwa nadharia, bado anakabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela katika kila kosa la kodi na miaka 10 jela kwa kosa la silaha.

Makubaliano ya kuepuka kifungo yanahitaji kuthibitishwa na jaji anayesikiliza kesi hiyo, ambaye pia ataamua aina ya adhabu.

Chapisha Maoni

0 Maoni