Mmoja wa wanaume
watano waliothibitishwa kufa kwenye nyambizi ya Titan Dubai, Hamish Harding
(58), alipanga kuja kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na wanafamilia yake na
washkaji zake wanaofikia 20 Julai, 2023, baada ya matamanio yake hayo awali
kukwama kutokana na Uviko-19.
Waliokufa ni
Hamish Harding, 58, Shahzada Dawood, 48, na mwanae Suleman Dawood, 19,
Paul-Henri Nargeolet, 77, pamoja na Stockton Rush, 61.
Harding ana rekodi
tatu za dunia za Guinness, wakati mwaka 2021 aliweka rekodi ya kuwa mmoja wa
wanadamu waliofanikiwa kwenda sehemu ya chini kabisa duniani alipotembelea
handaki la baharini la #marianatrench akitumia saa 36 majini na chombo
kilichoitwa #challengerdeep.
Mwaka huu
Harding alipanga kufanya #royaltourtanzania, akidhamiria kufika kwenye kilele
cha juu zaidi duniani kilichosimama chenyewe kwa kufika@#mountkilimanjaro.
0 Maoni