Ndugu waomboleza waliokufa kwenye nyambizi Titan

 

Salamu za rambirambi zimeanza kutolewa baada ya wanaume watano waliokuwamo kwenye nyambizi ya Titan kufa.

Waliokufa ni Hamish Harding, 58, Shahzada Dawood, 48, na mwanae Suleman Dawood, 19, Paul-Henri Nargeolet, 77, pamoja na Stockton Rush, 61.

Familia zao zimekumbwa na majonzi makubwa, zikielezea safari yao ya mwisho ya uvumbuzi iliyotwa uhaia wao.

Chombo hicho cha roboti cha kuzama majini kilipata hitilafu kikiwa majini umbali wa mita 480 kutoka kwenye mabaki ya meli ya Titanic, siku ya Alhamisi.

Chapisha Maoni

0 Maoni