Yanga yapigwa faini ya zaidi ya milioni 82 CAF



Klabu  ya Yanga imetozwa faini ya jumla ya Dola 35,000 na CAF ambayo ni zaidi ya Shilingi 82 milioni kwa makosa mbalimbali yanayodaiwa kufanywa katika mechi yao ya robo fainali kati yao na Rivers United ya Nigeria.


Rivers United walitoa malalamiko yao siku moja kabla ya mechi hiyo baada ya kumaliza mazoezi yao uwanjani hapo.


Malalamiko ya Rivers kuwa gari yao ilivunjwa  vioo na kuibiwa dola 5000 huku wakidai pia kupuliziwa dawa.
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), iliyokutana Mei 4 mwaka huu, imeipiga faini Yanga kwa madai ya kuhusika kuwasha vitochi na kupiga mafataki uwanjani ambapo faini yake ni dola 10,000.


Faini nyingine ni Dola 25,000 kwa madai ya kupuliza dawa kwenye gari la timu ambalo walilitumia Rivers United walipokuwa mazoezini. Caf imeilekeza Yanga kulipa fedha hizo ndani ya siku 60 tangu kutolewa kwa adhabu hiyo.

Aidha Caf imetoa nafasi kwa Yanga kukata rufaa ndani ya siku tatu tangu kutolewa kwa adhabu hiyo na wakishindwa kukata rufaa ndani ya muda elekezi basi watatakiwa kulipa faini hiyo kama walivyoelekezwa.


Mechi hiyo ilichezwa  Aprili 30, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam na kutoka bila kufungana na Yanga kutinga nusu fainali kwa ushindi goli 2 za ugenini.

Chapisha Maoni

0 Maoni