Undani lifti iliyojeruhi 7 Millenium Tower Makumbusho

 

Mkaguzi Msaidizi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  Patrick Mohamed amesema kudondoka kwa lifti katika Jengo la Milenium Tower kumetokana na kuzidiwa kwa uzito.


Akizungumza baada ya zoez la uokoaji amesema taharuki hiyo imesababishwa la lifti kushuka bila breki kutoka ghorofa ya kumi mpaka chini kutokana na uzito uliopitiliza.



Amesema licha ya kutokea kwa changamoto hiyo lift hiyo ilikuwa katika matengenezo kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita.


Amesema ilikuwa imebeba watu zaidi ya 10 ambapo waliojeruliwa ni 7 na wamepelekwa katika hospitali ya Hubert Kairuki kwa matibabu zaidi, huku akitoa wito kwa wamiliki kufanya majaribio ya lifti kwa kutumia mizigo au nyenzo nyingine baada ya matengenezo ili kujiridhisha na uimara wake.



Kwa mujibu wa wakili Henry Mwinuka amesema suala la fidia kwa waathirika lipo kisheria lakini hii imekuwa ni kasumba kwa wamiliki kwa kutojali lakini fidia zipo kuna general damage na specific damage kutokana na maamuzi ya mahakama.


Na kuwa ni vyema wamiliki wazingatie na kuweka tahadhari katika majengo yao kwani madhara huwa ni makubwa ikiwa ni pamoja na  vifo na ulemavu wa kudumu.


Kwa upande wao wamiliki wa jengo hilo ambao ni Mtuko  wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema utachukua jukumu la kurekebisha hitilafu zilizojitokeza katika jengo la Millennium Tower 2, lililopo Kijitonyama Dar es Salaam.

Taarifa ya PSSSF imesema kuwa kama wamiliki wa jengo watashirikiana na msimamizi wa jengo Ms. Prolaty Ltd ili kurejesha huduma zingine kama ilivyo awali.

PSSSF wameeleza kuwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi wanaendelea kuchunguza chanzo cha hitilafu hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni