Kumbe Feisal amegomea mshahara Yanga, Eng. Hersi afunguka

Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amefunguka kuhusu sakata la Feisal Salum maarufu Fei Toto na kusema mwaka 2020 alikuwa akipata mshahara wa shilingi 1,500,000 akaongezewa hadi milioni 4 na gharama ya usajili ilikuwa shilingi milioni 100.

Katika mahojiano yake na redio ya Clouds fm Eng. Hersi amesema kuwa klabu ilikubali  kumpa kiasi chote cha gharama ya usajili milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha jambo la familia yake tofauti na kiasi cha shilingi milioni 25 kwa kila mwaka.

Akijibu swali iwapo kama  Yanga ikiamua kujishusa na kumkubalia Feisal kuondoka, au Je iwapo Yanga itashtakiwa ikigoma? 

Eng Hersi amesema kwanza hilo ni suala la hisia “Hii ni taasisi na haina huruma inasimama kwa misingi ya sheria na inasimamiwa na kuheshimiwa sisi tumempa muda arudi atumikie mpaka mwaka Mei 30 2024, au pili aongezewe maslahi na tatu anaweza kufanya transfer (uhamisho)”.


Kuhusu mshahara wake “Sasa anapokea mshahara amepokea mpaka Januari ila Februari akaweka standing order kwenye akaunti yake na tulimuandikia kuwa atupe akaunti nyingine ili fedha zake zitumwe na hajajibu mpaka leo kwahiyo akitupatia akaunti fedha zote zitaingiziwa”.



“Sisi kama Yanga tunampenda na ni kijana mzuri na yupo katika nafasi ambayo anaweza kuendeleza nafasi yake” amesema Eng. Hersi.


Kuhusu sakata la mkataba amesema mkataba wa hali ya kawaida unaweza kuvunjwa isipokuwa lazima kuwepo na sababu za kuvunja mkataba sisi na Feisal hakukuwa na sababu za kuvunja mkataba.


Kwa mujibu ya kilichomo ndani ya makubaliano hakuna sababu ya kuvunja mkataba na baada ya rufani mara tatu kamati ilipiga chini maombi yote kwakuwa ilijiridhisha kuwa hakuna ukiukwaji wa mkataba.


Mikataba inatoka FIFA inatoa miongozo CAF na inakuja kwa uongozi wa klabu na katika mikataba kuna vitu muhimu ambavyo ni maslahi binafsi ikiwemo gharama za usajili na mshahara na muda wa mkataba.

Chapisha Maoni

0 Maoni