Siri nzito watu wanne wa familia moja wafariki kwa kuungua moto

Watu wanne wa familia moja Kijiji cha Malola B Kata ya Malola Tarafa ya Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wamefariki baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuungua Moto usiku wa kuamkia Mai 5, 2023.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amefika eneo la tukio na kuthibisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema bado uchunguzi unaendele ili kubaini chanzo cha tukio hilo.



Aidha Kamanda amewataja waliofariki ni Amani Malekela (72) ambaye ni Baba wa familia hiyo, Habiba Aman ( 10), Sadick Amna (8) na Bahati Aman.

SHUHUDA 

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mjukuu wa  marehemu aliyefahamika kwa jina Mwanjaa Madumba  amesema majira ya saa  saba usiku wa kuamkia May 5,2023 akiwa amelala aliona moshi mkubwa unatokea upande wa chumba cha babu yake alikolala na Watoto wake watatu.


Baada ya kupiga kelele Watu walifakiwa kuzima moto huo na walipojaribu kufungua mlango wa chumbani walikuta watu hao wanne wameteketea kwa moto.


Babu Aman Malekela ambaye sasa ni marehemu miaka kadhaa iliyopita alitengana na mkewe na kubakia na watoto wake hao ambao wameteketea kwa moto.

Chapisha Maoni

0 Maoni