Feisal Salum arudishwa Yanga Kamati yatupilia mbali maombi yake

 

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la soka Tanzania Soka Tanzania (TFF), imetupilia mbali ombi la Feisal Salum kuhusu kuvunja mkataba na klabu ya Yanga ambapo imesisitiza mkataba wake na klabu hiyo ni halali hadi mwaka 2024.


Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na mawasiliano wa TFF  Clifford Ndimbo imetolea ufafanuzi maamuzi ya kamati hiyo baada ya mchezaji Feisal  Salum kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Yanga.



Baada ya kupitia na kutafakari hoja za Feisal Salum na Wanasheria wake na Yanga na Wanasheria wake, Kamati imetupilia mbali shauri hilo na kwamba ilishaamua kuhusiana uhalali wa mkataba wa mchezaji huyo na Yanga.


“Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazotawala uvunjaji wa mikataba, mchezaji lazima aanze majadiliano na club yake ambayo ndio ina haki nae”

Chapisha Maoni

0 Maoni