Wabunge wa mwambao wapinga uagizaji wa chumvi nje ya nchi

Wabunge wa mwambao wa bahari ya Hindu ikiwemo Lindi na Mtwara wameomba serikali kusitisha kutoa vibali vya kuagiza chumvi kutoka nje  ya nchi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wabunge hao wakati wakichangia hoja katika rasimh ya bajet ya wizara ya uwekezaji viwanda na biashara ambapo  wamesema ni muhimu kusitisha ili kulinda viwanda vya ndani na kuongeza ajira kwa wazawa.


Hassan Mtenga ni mbunge wa Mtwara Mjini amesema chumvi ya Tanzania imekosa soko  kwasababu ya mwekezaji mmoja tu na kuwa suala hilo sio sawa.


Stanslaus Nyongo ni mbunge wa Mtwara Mashariki amesema “tunaingiza asilimia 70 ya chumvi kutoka nje ambapo hapa nchini chumvi inajitosheleza” 

Akijibu hoja hiyo Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema serikali ilishasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza chumvi nje ya nchi na wizara ya uwekezaji na wizara ya madini hakuna kibali kilichotolewa mpaka sasa.


Uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ndani unatajwa kuwa tani laki tatu na mahitaji yakiwa ni laki mbili hamsini elfu.

Chapisha Maoni

0 Maoni