Napoli waukwaa ubingwa wa Sirie A

 


Timu ya Napoli imetwaa taji la ligi ya Italia ya Sirie A kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 33 baada ya kutoa sare na Udinese katika dimba la Dacia Arena na kuibua sherehe kubwa nyumbani Naples.

Kwa mara ya mwisho Napoli ilitwaa ubingwa wa ligi hiyo mnamo mwaka 1990, ambapo Diego Maradona ndiye aliyekuwa chachu kwa timu hiyo kutwaa kombe lakwanza.

Mchezaji wa Napoli Victor Osimhen alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya 52 baada ya Sandi Lovric kuipatia Udinese goli la kuongoza. 

Baada ya kusawazisha Napoli iling'ang'ania kutoka na pointi moja katika mchezo huo iliyokuwa inaihitaji ili kutawazwa kuwa mabingwa wa Serie A kwa msimu huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni