Trump ajichanganya mahakamani kesi ya ubakaji

 


Katika hali isioyakawaida Donald Trump ameonekana kujichanganya mahakamani baada ya kufikiri mwanamke anayemshtaki kwa kumbaka E Jean Carrol, kuwa ni mtalaka wake Marla Maples

Trump aliyekuwa rais wa Marekani anasikika kwenye mkanda wa video uliochezwa Mahakamani akiiuliza "yule sio Marla?", kisha wakili wake akamsahihisha kwa kumuambia "Hapana ni Carrol".

Bi. Carrol mwenye umri wa miaka 79 anamtuhumu Trump miaka 76 kwa kumshambulia huko New York City mnamo mwaka 1990, tuhuma ambazo Trump amezikanusha.

Mawakili wa Carroll amesema kujichanganya kwa Trump baada ya kuona picha ya Carroll kunakinzana na kauli yake kuwa mwanamke huyo sio hadhi yake, kauli ambayo amekuwa anaitoa tangu kuibuka kwa tuhuma dhidi yake mwaka 2019.

Pande zote mbili zimekamilisha kutoa ushahidi wao katika kesi hiyo, na kumaliza uwakilishaji wa hoja zoa mbele ya mahakama wakingojea kutolewa maamuzi ya mahakama, upande wa Trump hakuwa na mashahidi katika kesi hiyo.

Trump amewaambia waandishi wa habari anafikiria kukatisha safari yake ya kwenda kucheza golf Ireland ili amfariji Carrol mahakamani. "Nitarejea mapema kwa kuwa mwanamke huyu ametoa madai ambayo ni ya kupotosha kabisa," alisema Trump.


Chapisha Maoni

0 Maoni