Rais Samia kushiriki mkutano wa dharura wa Troika plus wa SADC

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili  nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIC)


Mkutano huo utajadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Watoto Miranda Masatu wa kwanza kulia, pamoja na Samra Mdee mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia tarehe 07 Mei, 2023. Wa kwanza kulia ni Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob akishuhudia tukio hilo.

Picha na Ikulumawasiliano

Chapisha Maoni

0 Maoni