Rais Samia atuma salamu kwa Mawaziri wa Michezo Kanda Afrika


Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametuma salamu kwa njia ya video fupi ambapo amewakaribisha  Mawaziri wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV kwenye Mkutano wa kwanza wa Kanda hiyo kufanyika hapa nchini.

RAIS SAMIA VIDEO

"Huu ni mkutano wa kwanza wa kihistoria wa Kanda ya IV kufanyika katika ardhi ya Tanzania tunawakaribisha Wajumbe wote wa  Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV hapa nchini kwetu ambayo ni Nchi ya amani na ukarimu ikiwa na vivutio vingi vya Utalii Bora Duniani" amesema  Rais Dk Samia.



Aisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan  amewahakikishia wajumbe wa wajumbe wote wa  Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV kuwa Tanzania ipo tayari kuwa Makao Makuu ya Baraza hilo.

Miongoni  mwa agenda za mkutano huo ni kuchagua nchi ambayo itakuwa Makao Makuu ya Baraza hilo.

Chapisha Maoni

0 Maoni