TCAA yatoa ufafanuzi kugeuza kwa ndege iliyobeba timu ya Yanga


 Mamlaka  ya usafiri wa anga (TCAA) imetoa ufafanuzi kugeuza kwa ndege iliyobeba timu ya Yanga ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa TCAA Hamza Johari ikifafanua kuhusu tukio la Mei mosi ambapo ndege ya Precision air ilishindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kurudi Dar es Salaam.

Johari amesema mamlaka hiyo  itawachukulia hatua wote waliohusika ikiwa kulikuwepo na ukiukwaji wa uendeshaji katika uwanja wa ndege wa Dodoma.


Johari amesema mnamo May 01, 2023, ndege ya Precision Nambari. PW 602, iliondoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA ), saa 12:11 jioni kwa safari ya saa moja kuelekea Dodoma ikiwa na abiria 72, ilitarajiwa kutua uwanja wa ndege wa Dodoma saa 01:13 usiku ambao ni muda zaidi ya masaa ya uwanja huo kufanya kazi. 


“Uwanja wa ndege wa Dodoma hufungwa saa 12:30 jioni kutokana na changamoto za miundombinu zilizopo kwa sasa”


“Ilipofika majira ya saa 12:48 jioni Rubani wa ndege hiyo alilazimika kugeuza na kurudi uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kushauriwa na muongoza ndege wa zamu, taarifa za awali za uchunguzi wa tukio hilo zimeonesha kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kiuendeshaji”


Ndege hiyo siku ya Mei 1 ilikuwa pia imebeba abiria na miongoni mwao ni wachezaji wa Yanga waliokuwa wakisafiri kwaajili ya maandalizi ya mechi kati yao na Singida Big Stars itakayopigwa May 4 uwanja wa Liiti.

Chapisha Maoni

0 Maoni