Rais Samia akonga nyoyo za wafanyakazi aahidi kupandisha mishahara,madaraja

 


Rais  Samia Suluhu Hassan, amejibu hoja za wafanyakazi  na kusema kuwa hatatangaza hadharani suala la kupandisha mshahara, lakini amewaeleza wafanyakazi kuwa  mambo mazuri yapo na mishahara itapanda kila mwaka.


Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2023, yaliyofanyika kitaifa mjini Morogoro , 2023, Rais Samia amesema kujitoa kwa wafanyakazi kwa bidii kutasaidia kulijenga Taifa.


Akizungumzia nyongeza ya mishahara na posho, Rais Samia amesema zipo taasisi ambazo zilishindwa kutekeleza agizo  la kutoa nyongeza za psoho kwa kuwa wakati anatoa agizo hilo bajeti ilikuwa imeshapita, kwa maana hiyo mavuno ya posho hizo yatakuwa kwenye bajeti ya mwaka huu, 2023/2024.



 Amesema, mbali na upandishaji wa posho, mwaka huu pia ataendelea  kupandisha madaraja, vyeo na madaraja mserereko upo mwaka huu.

“Lakini niseme pia kuna nyongeza za mishahara ambazo muda mrefu zilisitishwa, nimeona mwaka huu tuzirudishe. Kwa hiyo wafanyakazi wote mwaka huu nyongeza za kila mwaka zitakuwepo na itakuwa hivyo kila mwaka.

“Nashukuru Tucta mwaka huu wamenielewa hawakuja na mdomo mkali wa moto mara hii wamekuwa wapole, kwa hiyo waliyozoea nitangaze hapa ili wajue kiasi gani, ili  wapandishe bei madukani sitatangaza,  ili mwenendo wa bei uwe salama, tutapandisha pole pole mambo mazuri yapo ila hatutayatangaza hapa, mambo ni moto, mambo ni fire, suala lililoibua shangwe kwa wafanyakazi.



Akizungumzia hoja ya kodi na marupurupu ya makato kwa wakati pamoja hadi zawadi zinakatwa kodi, ameelekeza Waziri wa Utumishi na Waziri wa Fedha kukaa kuangalia yale yanayopaswa kukatwa kodi yakatwe na yasiyofaa yaondolewe.



“Leo nimeshuhudia mtu anatoka na milioni 12 hapa kwa nini asikatwe kodi, hiyo kodi itarudi kwenye kufanya shughuli nyingine, hivyo naliacha kwa Waziri wa fedha na Waziri wa Utumishi yanayopaswa kulipa kodi yalipwe yanayofaa  kuondolewa yaondolewe,”amesisitiza Rais Samia.



Aidha ametoa siku 60 kwa waajiri kulipa malimbikizo ya bima za afya, ili wafanyakazi wao waweze kupata stahiki zao za matibabu.

Kuhusu waajiri wa kutopeleka michango katika mifuko ya jamii na michango ya bima za afya.

Chapisha Maoni

0 Maoni