Prof Jay aanza kutengeneza shavu rasmi

 

Msanii nguli wa muziki wa Bongofleva na mwanasiasa Joseph Haule maarufu Profesa Jay ameonekana hadharani baada ya miezi kadhaa ya matibabu.



Kwa mara ya kwanza kujitokeza ilikuwa ni Mwezi May ambapo aliandika ujumbe mzito wenye shukrani kwa watu mbalimbali waliohusika kupigania uhai wake akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.



Leo May 22 ameonekana katika viunga vya Tabata Segerea na kuandika ujumbe “Leo nimeanza rasmi operation ya rudisha shavu nikiwa na mdogo wangu wa damu Blackchata” ameandika kupitia Instagram 


Huu hapa waraka wa Prof Jay alipojitokeza hadharani kwa mara ya kwanza 

Hakika ni jambo jema kwa aliyekuwa dhaifu kurejea katika afya na kuendelea na majukumu yake.


Tunamtakia kila la kheri katika mapambano yake na labda tutegemee lolote kutoka studio hata katika ulingo wa siasa.


Prof Jay aliwahi kuwa mbunge wa Mikumi kupitia CHADEMA.

Chapisha Maoni

0 Maoni