Mwanamuziki Tina Turner afariki dunia

Mwanamuziki Tina Turner, ambaye vibao vyake vikali vya The Best na What's Love Got to Do With It vilimpatia umaarufu mkubwa, amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 83.

Turner alikuwa anakabiliwa na matatizo kadhaa ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni yakiwemo ya saratani, kiharusi na figo kushindwa kufanyakazi.

Mwanamuziki huyo alipata umaarufu pamoja na mumewe Ike katika miaka ya 1960 kwa nyimbo zao zikiwemo za Proud Mary na River Deep, Mountain High.

Mnamo mwaka 1978 alitengana na Ike ambaye alikuwa akimfanyia vitendo vya ukatili, na kuendelea kuimba peke yake na kupata mafanikio zaidi katika miaka ya 1980.

Turner aliyepachikwa jina la Malkia wa Rock 'n' Roll, alikuwa maarufu kwa uchezaji wake wa mitego na kutumia nguvu jukwaani pamoja na sauti yake kali.

Chapisha Maoni

0 Maoni