Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi amehudhuria dhifa ya chakula cha mchana iliyokuwa
imeandaliwa na Mfanyabiashara maarufu kutoka Qatar Feisal Bin Qassim Bin Feisal
Bin Thani Bin Qassim Bin Mohamed Al Thani.
Mfanyabiashara huyu ni mmiliki wa hoteli 30 kubwa duniani na
makumbusho ambayo yana vitu vingi vya kusisimua vya zamani.
Baada ya dhifa ya chakula cha mchana, Rais Dk Hussein Ali
Mwinyi, pamoja na Mama Mariam Mwinyi na ujumbe wake, walipata fursa ya
kutembezwa ndani ya makumbusho hayo, Makumbusho hayo yana mkusanyiko mkubwa wa
vitu vya kihistoria kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Moja kati ya vitu vilivyomvutia Rais Mwinyi ni noti ya
zamani ya Zanzibar iliyotumika mwanzoni mwa mwaka 1916.
Kupata noti hiyo katika makumbusho ya nchi ya Qatar
kunadhihirisha ushawishi na utajiri wa historia ya Zanzibar na thamani yake
katika historia ya dunia.
Mbali na noti hiyo, makumbusho hayo pia yanahifadhi aina
mbalimbali za magari ya zamani, yakiwemo yale yaliyotengenezwa mnamo mwaka
1890.
Noti ya zamani ya Zanzibar iliyotumika mwanzoni mwa mwaka 1916
0 Maoni