Man United hao UEFA, Liverpool waangukia Ligi ya Europa

Manchester United imekata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya, huku ikiwa imebakiza mchezo mmoja mkononi, baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Chelsea.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Old Trafford Casemiro alifunga goli la kwanza kwa kichwa na kisha Anthony Martial kufunga la pili akipewa pande na Jadon Sancho.

Bruno Fernandes aliifungia goli la tatu Manchester United, kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa madhambi na mchezaji wa Chelsea Wesley Fofana.

Makosa ya pili ya Fofana yalizalisha goli la nne lililofungwa na Marcus Rashford, kabla ya Joao Felix kuifungia Chelsea goli pekee katika dakika za mwisho.

Kwa matokeo hayo inamaanisha Manchester United, imewasukuma wapinzani wao Liverpool kwenye ligi ya Europa katika msimu ujao.

 

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, amesema imewachanganya klabu hiyo kukosa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu ujao, na kuongeza kuwa hakuna cha kujitetea kwa hilo.

Chapisha Maoni

0 Maoni