Fei Toto akumbuka mashuti, ashusha ujumbe mzito

 

Kiungo wa Yanga , Feisal Salum maarufu kama Feo Toto ametoa ya moyoni kutaka  kurudi kusakata kabumbu baada kipindi kirefu kuwa nje ya uwanja kufuatia mgogoro wake na klabu yake.


Feisal ameandika kupitia mtandao wa Instagram, kuwa amebakisha hatua chache ili kufanikisha nia yake ya kufungua mashitaka katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).


“Ndugu zangu Watanzania, natamani kurudi uwanjani na kuendelea kuwafurahisha wapenda soka, nimebakisha hatua chache, nisaidieni niweze kukamilisha nia yangu ya kwenda CAS na kupata haki ya kurudi tena uwanjani".



“Nimekumbuka Nyakati bora, nimekumbuka kupiga mashuti yangu ya mbali, nimekumbuka kufurahia na mashabiki wa soka. Fei Toto ni mmoja tu, msaidie arudi uwanjani kwa Haki inayotaka kudhulumiwa,” ameandika Fei Toto.

Chapisha Maoni

0 Maoni