NBA yaipiga faini ya dola laki 7 Dallas Mavericks

 

Dallas Mavericks wamepigwa faina ya dola 750,000 na NBA kwa kosa la kuwapumzisha wachezaji wake muhimu katika mchezo dhidi ya Chicago Bulls licha ya kuwapo kwenye kuwania play-off .

Katika taarifa yake NBA imesema Mavericks wameonyesha nia ya kupoteza ili kuimarisha nafasi ya kuchaguliwa kumi bora wakati wa upangaji timu majira ya joto.

Makamu wa Rais wa NBA Joe Dumars amesema kitendo ha Mavericks kimewaangusha mashabiki wa NBA na ligi hiyo.

Katika mchezo huo uliochezwa Aprili 7 Mavericks walifungwa kwa alama 115-112 na Chicago Bulls.

Dallas imesema wachezaji wake Kyle Irving, Tim Hardaway Jr na Maxi Kleber wote walikuwa ni majeruhi wakati Josh Green na Christian Wood walikuwa wamepumzishwa.

Chanzo:BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni