Tanzania yaonesha utayari wa AFCON 2027

Waandishi nguli wa habari za michezo na burudani kutoka sehemu mbalimbali duniani walioko nchini Tanzania kwa ziara ya kiutalii na kufuatilia maandalizi ya AFCON 2027,  2026, wametua jijini Arusha na kutembelea uwanja mpya wa mpira utakaotumika katika mashindano hayo.

Waandishi hao wamevutiwa na uwanja huo pamoja na maandalizi yanayoendelea, wakieleza kuwa Tanzania ipo tayari kuandaa AFCON 2027.

Wamesema uwepo wa uwanja huo Arusha unatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki wa soka kuunganisha burudani ya mpira na utalii, kwa kuwa jiji hilo liko karibu na vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa Arusha, Tarangire, Mto wa Mbu na maeneo mengine ya kuvutia.

Ziara hiyo pia imewashirikisha waandishi na influencers wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kutoka mataifa mbalimbali, wakiwemo wawakilishi kutoka Sporty TV ya Hispania, TRT ya Canada, NWE Media ya Marekani, pamoja na influencers kutoka Uingereza na Ufaransa.

Kupitia majukwaa yao ya kidijitali, wageni hao wanaendelea kushirikisha dunia uzuri wa Tanzania, vivutio vyake vya utalii na maandalizi kuelekea AFCON 2027, hatua inayotarajiwa kuongeza uelewa na hamasa ya kimataifa kuhusu Tanzania kama kituo cha michezo na utalii.



Chapisha Maoni

0 Maoni