Mfungwa aliyechomwa sindano za sumu afe atibiwa kuokoa maisha yake

Christa Pike, mwanamke wa Marekani aliyetiwa hatiani kwa mauaji, amelazwa hospitalini na anapatiwa matibabu ya kuokoa maisha baada ya mamlaka za Tennessee kushindwa kumuua kwa sindano yenye sumu.

Kesi ya Pike, ambaye jaribio lake la kunyongwa kwa sindano tayari lilikuwa limeibua mvutano mkubwa wa kisheria, sasa imeibua maswali kadhaa.

Maswali hayo yanahusu kilichokwenda vibaya, nini kitafuata na kwa wapinzani wa adhabu ya kifo, wasiwasi mpya kuhusu mateso anayoweza kupitia mfungwa pale utekelezaji wa hukumu ya kifo unaposhindikana kwenda kama ulivyopangwa.

Pike mwenye umri wa miaka 50 alihukumiwa kifo mwaka 1996 kwa mauaji ya Colleen Slemmer, mwenye umri wa miaka 19, katika shambulio alilolitekeleza pamoja na mpenzi wake wa wakati huo, Tadaryl Shipp.

Alipangwa kuuawa Jumatano jioni kwa saa za eneo hilo. Matumizi ya sindano za dawa za kumuua yaliruhusiwa na Mahakama Kuu ya Marekani dakika za mwisho baada ya mfululizo wa mapambano ya kisheria.

Pike alidungwa sindano mbili za dawa ya pentobarbital, ingawa mawakili wake walisema dawa hizo zilishindwa kusimamisha mapigo ya moyo wake na kwamba bado aliweza kusikika akikoroma.

Chapisha Maoni

0 Maoni