Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan imempendekeza Deogratius Ndejembi (43) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hilo limetangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha Rose-Migiro usiku wa Jumatano, Agosti 26, 2026, ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Dkt. Migiro amesema baada ya kupendekezwa jina hilo litapelewa bungeni kwa hatua zingine.
Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati anachukua nafasi ya Dkt. Nchimbi, ambaye alitangaza kujiuzulu.
Wakati huo huo, aiyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amefukuzwa uanachama wa chama hicho.
Dkt. Nchimbi amefukuzwa unachama siku moja baada ya kumwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan kumwomba kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais ambapo ombi hilo lilikubaliwa.
Uamuzi wa kufukuzwa uanachama, umetangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Asha Rose- Migiro alipozungumza na waandishi wa habari, ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Ambapo alikuwa akitoa maazimio ya vikao vya kamati kuu na Halmashauri Kuu vilivyokutana jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi hadi usiku wa Jumatano.
Dkt. Migiro amesema kulikuwa na ajenda ambazo zilijadiliwa na miongoni ni suala la maadili lililokuwa linamkabili mwanachama wetu Dkt. Nchimbi na vikao vyote vilijadili.

0 Maoni