Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kitaifa katika Uwanja wa Mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Rais Dkt. Samia aliwasili katika viwanja vya maadhimisho na kupokelewa kwa heshima rasmi za kijeshi, kabla ya kupokea heshima ya wimbo wa Taifa wa Tanzania na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika kilele cha maadhimisho hayo, Rais Dkt. Samia aliweka mkuki na ngao kwenye Mnara wa Mashujaa, ikiwa ni ishara ya heshima kwa mashujaa waliolitumikia Taifa kwa ujasiri na uzalendo.
Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na
viongozi wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, wanajeshi wastaafu,
viongozi wa dini, wananchi na wageni mbalimbali. Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa
huadhimishwa tarehe 25 Julai ya kila mwaka kwa heshima ya mashujaa waliopigania
uhuru na wale waliojitolea kulinda amani, usalama na maslahi ya Taifa.




0 Maoni