Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amekabidhiwa zawadi ya kitabu kiitwacho ‘The Game of the Impossible’ na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Bi. Catherine Sungura.
Kitabu hicho, kilichoandikwa na PEMANDU Associates ya Malaysia, kinaelezea uzoefu wa taasisi hiyo katika kuiwezesha Malaysia kutekeleza mageuzi makubwa ya kitaifa kupitia mifumo madhubuti ya utekelezaji wa sera, mipango na usimamizi wa matokeo.
Kitabu hicho kinatarajiwa kuwa rejea muhimu wakati TARURA inaenda kutekeleza Mpango Mkakati wake wa tatu wa mwaka 2026/2027-2030/2031.

0 Maoni