Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ)imesema inaunga mkono ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza
Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ikiwataka
wanasiasa kuacha kuwashawishi vijana kujiingiza katika vurugu za
kisiasa zinazohatarisha maisha yao na usalama wa taifa.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar, Hamza Hassan Juma, wakati akitoa maoni ya serikali kuhusu
ripoti hiyo iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman
ambayo tayari imewasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Juma
alibainisha kuwa tume imefanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya
vurugu yaliyojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Dar es
Salaam, Mwanza, na Arusha, na kubaini kuwa baadhi ya wanasiasa
walitumia ushawishi wao kuwahusisha vijana katika vurugu hizo kwa
lengo la kuvuruga mchakato wa uchaguzi, jambo lililosababisha
uharibifu wa mali na kupotea kwa maisha ya baadhi ya
wananchi.
Waziri Juma aliwaomba wanasiasa kufanya siasa za
kujenga nchi na kuhubiri uzalendo badala ya kuwashawishi vijana
kuingia katika vurugu ambazo athari zake ni kubwa kwa taifa na kwa
maisha yao binafsi, huku akisisitiza kuwa nguvu kazi hiyo inapaswa
kuelekezwa katika fursa za uzalishaji mali na ujasiriamali.
Alisema
changamoto ya ukosefu wa ajira isitumiwe kama kigezo cha kuwatumia
vijana kwa maslahi ya kisiasa, bali sekta binafsi ipewe nafasi ya
kuwasaidia kujiajiri na kujitegemea kiuchumi ili kuimarisha ustawi
wao. Aidha, aliwasihi vijana wenyewe kuwa macho na kuepuka
kushawishiwa kujiingiza katika vurugu, na badala yake wazingatie
uzalendo, kuheshimu sheria za nchi, na kushiriki kikamilifu katika
shughuli mbalimbali za maendeleo ya kitaifa.
Kwa upande wa
Zanzibar, Waziri huyo alieleza kuwa serikali imejifunza kutokana na
matukio ya nyuma na imekuwa ikiendelea kutoa elimu kwa vijana kuhusu
umuhimu wa kulinda amani na utulivu wa nchi, jambo lililopelekea
uchaguzi mkuu uliopita visiwani humo kufanyika kwa amani kubwa na
kupongezwa na waangalizi wa ndani na nje ya nchi.
Alisema
vurugu zilizotokea kabla na baada ya uchaguzi mkuu zinapaswa kuwa
fundisho la umuhimu wa vijana kuwa wazalendo wa kweli na kujiepusha
na ushawishi wa wanasiasa wenye tamaa ya madaraka ambao wako tayari
kuhatarisha amani ya nchi kwa maslahi yao binafsi.a na kazi nzuri
anayoifanya katika kuiongoza nchi.
Alisisitiza umuhimu wa
kuheshimu mamlaka, kulinda mali za umma na kuhakikisha tofauti za
maoni zinatatuliwa kwa njia za amani na kisheria.

0 Maoni