Maadhimisho
ya siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika katika Makumbusho ya
Urithi Jiopaki mjini Karatu tarehe 5 Mei, 2026 yameyakutanisha
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ikiwa na lengo la
kuwarithisha kizazi kipya historia na elimu ya urithi na
utamaduni.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dkt Lameck Karanga
amesema uwepo wa makabila hayo, historia yao pamoja na kuenzi
tamaduni zao ni utajiri mkubwa kwa Tanzania na kutoa wito kwa wadau
na jamii kwa ujumla kuendelea kulinda maeneo ya urithi wa dunia na
kuibua maeneo mapya yatakayoingizwa katika orodha ya Urithi wa Dunia
ili kuongeza thamani ya ubora wa kipekee ulimwenguni (Outstanding
Universal Value) na kuvutia wageni wengi zaidi.
Naibu Kamishna
wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii Ngorongoro Joas Makwati
ameeleza kuwa mamlaka itaendelea kuongeza juhudi za kulihifadhi eneo
la Ngorongoro ambalo ni urithi wa dunia na kultangazia zaidi kama
eneo pekee lenye Ushahidi wa kisayansi kuhusu historia ya binadamu
unaoeleza kuwa binadamu kwa kuthibitishwa na ugunduzi wa masalia ya
binadamu wa kale na zana za mawe zilizopatikana katika bonde la
Olduvai.
Kwa upande wake Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya
UNESCO Tanzania Dkt. Khamis Said ameeleza kuwa tangu Tanzania ijiunge
na UNESCO imepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuridhia
mikataba kumi (10) ya UNESCO,Kuwepo kwa Hifadhi Hai za Mwanadamu na
Mazingira sita (6) na Kuwepo kwa maeneo saba (7) ya urithi wa
Dunia.
Kauli mbiu ya siku ya urithi wa dunia kwa mwaka huu ni
“Kusherekea siku ya Urithi wa Dunia na kukuza Viongozi wa baadaye”.
(Celebrating Africa’s Heritage, Mentoring the Leaders of Tomorrow).

0 Maoni