WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu
Nchemba, leo Mei 10, 2026 amewasili Nairobi, Kenya ambako anatarajia
kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia
Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa
(Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and
Growth Summit) utakaofanyika Mei 11–12, 2026.
Lengo la
mkutano huo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na
Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia,
nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na
viwanda.
Aidha, mkutano huo unalenga kukuza uwekezaji mpya
kati ya Afrika na kampuni za Ufaransa, kujenga ushirikiano unaotajwa
kuwa wa usawa, pamoja na kujadili mageuzi ya mfumo wa fedha na
maendeleo endelevu ya Afrika.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na
Serikali unawakutanisha wadau wa maendeleo, wawekezaji pamoja na
sekta binafsi, na umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Rais wa Jamhuri
ya Kenya, Mheshimiwa William Samoei Ruto, na Rais wa Jamhuri ya
Ufaransa, Mheshimiwa Emmanuel Macron.


.jpeg)
0 Maoni