Msimu wa tano wa
Great Ruaha Marathon (GRUMA) umezinduliwa rasmi leo, tarehe
28/04/2026 mkoani Iringa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Kheri James, katika
Mkutano wa waandishi wa habari uliyowakutanisha wadau mbalimbali wa
utalii, michezo na uhifadhi, ukiwa ni mwanzo wa maandalizi wa mbio
hizo zitakazofanyika tarehe 4 /7/2026 ndani ya Hifadhi ya Taifa
Ruaha.
Great Ruaha Marathon si mbio tu, ni uzoefu wa kipekee
unaounganisha shughuli za utalii ikiwa ni pamoja na matembezi ya
miguu, (walking safari), Kuvua Samaki (sport fishing), kuendesha
baiskeli (cycling) kwa siku ya tarehe 3/7/2026 pamoja na mashindano
ya mbio za 5KM, 10KM na 21km kwa siku ya tarehe 4/7/2026 yote
yakifanyika kwenye mandhari halisi ya asili.
Hakika ni ku-vibe na kutalii!
Usipange kukosa!
Jisajili sasa 👉🏽www.greatruahamarathon.co.tz
Pia unaweza jisali kupitia TANAPA GO APP!
#Utalii #GreatRuahaMarathon #TanzaniaParks #RuahaNationalPark #Kamwene #DestinationTanzania


0 Maoni