MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa Kitaifa ikiwa ni namna muhimu ya kuwaenzi waasisi wa Muungano, Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.
Makamu wa Rais amesema ametoa msisitizo huo, wakati wa Tamasha la Usiku wa Mtanzania ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano, lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Amesema ni msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vijana na watanzania kwa ujumla kuhusu kuwa na mshikamano kulinda umoja na amani.
“Mheshimiwa Rais anasema kwenye umoja, kwenye amani tunakwenda vizuri, isipokuwa tunachangamoto kwenye mshikamano, kwahiyo Mheshimiwa Rais anawaomba Watanzania wote watafakari na kujielekeza katika kujenga mshikamano wa nchi yetu,” alisema Dkt. Nchimbi na kuongeza,
“Na mimi naungana na Mheshimiwa Rais katika kuwaomba kwamba namna pekee ya Baba wa Taifa Malimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume ni kuhakikisha kwamba tunaulinda Muungano wetu, tunalinda mahusiano yetu tunalinda mshikamano wetu.”
Makamu wa Rais amewasihi watanzania kutafakari na kujielekeza katika kujenga mshikamano ni kuhakikisha Muungano unalindwa.
Amesisitiza umuhimu wa kuvumiliana katika utoaji wa mawazo,kushauriana kujenga utaratibu wa kukubaliana hata katika masuala yanayotoafutiana mawazo.
#UmojaWetuNdiyoNguvuYetu
#turidhiane

0 Maoni