DC Msando awataka vijana kuwa wazalendo, walinde amani na utulivu

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando amewataka vijana kuwa wazalendo kwa Taifa lao kwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kudumisha amani na utulivu sanjari na kupinga vitendo vya rushwa.

Msando ameyasema hayo wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vijana ambapo amesema vijana ni mhimili muhimu kwenye maendeleo ya Taifa hivyo amewasisitiza kujiunga na jeshi la akiba na mafunzo ya JKT ili kupata ukakamavu na elimu ya uzalendo.

Amesema kwa hali inayoendelea duniani kwa sasa taifa linahitaji vijana wazalendo, wakakamavu watakaolilinda taifa lao, hivyo ni muhimu wakajiunga na JKT na kupata mafunzo ya ukakamavu.

Kwa upamde wake mmoja wa wawezeshaji aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba amewatala vijana kujifunza pia historia ya nchi yao ili kujua asili ya Taifa lao lakini pia wawe wabunifu ili kuwa na Taifa bora lenye amani na utulivu kwani vijana ndio nguvu kazi ya Taifa.

Naye Diwani wa Kata ya Mbezi Pius Nyantori aliposhiriki mafunzo hayo amewataka vijana kujitambua na kutumia vyema fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo zilizopo nchini ili kukua kiuchumi.

 #SisiNiWamoja

Chapisha Maoni

0 Maoni