Mkurugenzi Mkuu wa CDC ampongeza Rais Samia

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), Dkt. Jean Kaseya, akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuteuliwa kuwa Bingwa wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Mama na Mtoto pamoja na Afya na Haki za Uzazi na Jinsia. 

Uteuzi huo umeidhinishwa leo katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU kufuatia mapendekezo yaliyotolewa katika Ripoti ya mwaka 2025 ya Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Africa Centres for Disease Control and Prevention. Rais Dkt. Samia atahudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja. 

Kupitia wadhifa huo, Rais Dkt. Samia ataratibu na kuhamasisha juhudi za nchi wanachama wa AU katika kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuimarisha mifumo ya afya, na kulinda haki za afya ya uzazi barani Afrika.

Chapisha Maoni

0 Maoni