Mtoto aliyetelekezwa na wazazi wake baada ya kuzaliwa na uzito pungufu na ulemevu wa mikono katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Perpetua Amana amefariki baadaya ya kuugua ghafla katika kituo cha kulelea Watoto cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa Kg 1.2 na baadaye mama yake kutoweka na kumuacha wodini hivyo uongozi wa Hospiatali ya Amana uliamua kuchukua jukumu kumpatia uangalizi wa karibu na baadaye msamaria mwema aliamua kujitokeza na kuamua kumkumbati mtoto huyo aweze kupata joto la mama.
Mtoto huyo alizaliwa tarehe 13 Machi, 2025 na tarehe 26 Desemba, 2025 alipokea sakramenti ya ubatizo katika Kanisa Katoliki lililopo Msimbazi Centre na kupatiwa jina la Perpetua Amana.
Mtoto huyo aliendelea kulelewa hospitali hapo kwa takribani miezi kumi na moja na afya yake iliimarika vizuri na baadaye uongozi uliamua kumpeleka katika kituo cha kulelea Watoto Msimbazi Centre kwaajili ya uangalizi zaidi, tarehe 14 Februari, 2026 aliugua ghafla na kukimbizwa hospitali ya Amana ambapo wataalam walijitahidi kumpatia matibabu lakini tarehe 15 Februari, 2026 mtoto huyo alifariki dunia.
Perpetua Amana amezikwa tarehe 17 Februari, 2026 katika viwanja vya Makaburi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es Salaam.

0 Maoni