Alhaj Dkt. Mwinyi ahimiza huruma na mshikamano Ramadhani

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu wenye uwezo kuwasaidia wasio na uwezo ili nao waweze kutimiza ibada ya funga ipasavyo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Ameyasema hayo alipoungana na waumini katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa Msikiti wa Fatma Bint Mirdas, Kilimani. 

Amesisitiza kuwa makundi ya masikini, mafakiri, watu wenye ulemavu, wajane na mayatima yanahitaji kusaidiwa zaidi katika kipindi hiki. 

Aidha, amewataka wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula, akieleza kuwa Ramadhani si wakati wa kutafuta faida kubwa bali ni wakati wa kuhurumiana na kusaidiana, na kusisitiza umuhimu wa kudumisha au kushusha bei ili wananchi waweze kumudu mahitaji ya futari.



Chapisha Maoni

0 Maoni