Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza viongozi na wananchi mbalimbali katika maziko ya marehemu Joseph Abdallah Meza yaliyofanyika leo majira ya alasiri.
Mzee Joseph Abdallah Meza amefariki dunia tarehe 29 Januari 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Katika uhai wake, marehemu aliitumikia Serikali na Chama Cha Mapinduzi kwa uadilifu na weledi, akiwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo:
* Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) • Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) • Kamishina wa Bodi ya Mapato Zanzibar kabla ya kuwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) • Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC).
Marehemu alizaliwa tarehe 8 Agosti 1959 na kufariki tarehe 29 Januari 2026, akiacha mjane na watoto saba.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya familia, mtoto wa marehemu, Paulina Joseph Meza, amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa upendo na msaada mkubwa wa matibabu uliotolewa kwa marehemu, akimuelezea kama mtu wa watu na mwenye upendo mkubwa.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.

.jpeg)


0 Maoni