Wakati dunia ikitazama wapi pa kwenda kupata utulivu na
vivutio vya kipekee, staa wa muziki na mfanyabiashara mkubwa duniani kutoka
Marekani, Kanye West, ameweka wazi kuwa ndoto yake namba moja ni kuja Tanzania
kuupanda Mlima Kilimanjaro. Hii siyo bahati mbaya; ni ishara ya imani ambayo
watu mashuhuri duniani wanayo kwa nchi yetu.
Kwa hakika hii ni
habari kubwa na ya kimkakati sana kwa taifa letu. Kanye West siyo tu
msanii, bali ni "brandi" ya kimataifa yenye wafuasi mamilioni duniani
kote. Kitendo cha yeye kuweka Mlima Kilimanjaro kama kipaumbele chake namba
moja (Number 1 Bucket List) ni tangazo la bure lenye thamani ya mabilioni kwa
utalii wa Tanzania.
Kwa nini Kanye West anaitaka Tanzania? Jibu ni rahisi:
Amani. Utalii hauwezi kukua pasipokuwa na amani. Watu wanakuja Tanzania kwa
sababu wanajua ni nchi ya ukarimu, utulivu, na usalama. Mmarekani huyu anauota
mlima wetu kwa sababu anajua Tanzania ni "Visiwa vya Amani" katikati
ya misukosuko ya dunia.
Kutokana na ukweli huu tunapaswa kuwashinda wanaotutia doa.
Kuna wachache wanaotumia nguvu zao kutafuta manufaa binafsi kwa kujaribu
kuipaka rangi nchi yetu na kutafuta kutuvuruga. Lakini ukweli unabaki palepale:
Sisi tuko wengi, na wao ni wachache.
Sisi tunaopenda amani, mshikamano, na maendeleo ndio wenye
nchi hii. Tusiwaruhusu watu wachache wenye njaa ya madaraka au maslahi binafsi
watuharibie "brandi" ya nchi yetu ambayo sasa hata mastaa wakubwa
duniani wanaipigania kuja kuiona.
Tanzania ni Taifa Kubwa Kanye West kutaka kuja hapa ni
fursa ya kiuchumi. Itavutia wawekezaji, itatengeneza ajira kwa vijana wetu
(wapanda milima, mahoteli, na madereva), na kuitangaza Tanzania zaidi
kijiopolitika. Sisi ni Taifa kubwa lenye rasilimali nyingi, na kubwa kuliko
zote ni Amani yetu.
Swali kwa Watanzania: Mmarekani anatamani kuja kwetu kuona
fahari yetu, wewe Mtanzania unajivunia vipi rasilimali zako? Je, una mpango
gani wa kutembelea vivutio vyetu na kulinda amani inayovivuta hivi viumbe
vikubwa duniani kuja kwetu?

0 Maoni