Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, leo Desemba 30, 2025 ametembelea na kushuhudia zoezi la upigaji kura katika Jimbo la Fuoni lililopo Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Jaji Mwambegele amesema zoezi la upigaji kura katika jimbo hilo linaendelea vizuri, huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo licha ya kunyesha mvua asubuhi.
Aidha, Jaji Mwambegele amesema zoezi la uchaguzi wa Mbunge katika Jimbo la Siha lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania Bara, nalo linaendelea vizuri bila changamoto kubwa.
Ameeleza kuwa uchaguzi mdogo unaoendelea pia unahusisha kata tano za Tanzania Bara ambazo ni Kata ya Chamwino iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoa wa Morogoro; Kata ya Mbagala Kuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam; na Kata ya Nyakasungwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Mkoa wa Mwanza.
Kata nyingine ni Kata ya Masoko iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mkoa wa Mbeya, pamoja na Kata ya Ndono iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora.
Katika ziara hiyo,
Mwenyekiti wa Tume aliambatana na Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira.

0 Maoni