Ujumbe mzito umetolewa kwa kundi la vijana, ambao walitajwa kuingia kwenye mkumbo wa kuiga matukio mabaya bila kutambua athari zake. Vijana wanahimizwa kuona umuhimu wa kuketi na kutumia majukwaa yao ya kidijitali na kijamii kujadili umuhimu wa kulinda amani, maadili, na Utanzania wao.
Habib Sadick, dereva wa bajaji, anatoa Funzo muhimu
kwa vijana: "Kama kijana nilikuwa na wajibu wa msingi wa kupiga kura na
kuendelea na biashara... Lakini kilichotokea sijawahi kukiona. Sehemu kubwa ya
vijana waliofanya hivi vitu... Ni funzo kwa vijana kwamba vijana tusifanye kitu
chenye hasara kubwa katika maisha, usikifanye."
Salma Juma Kimaro anasisitiza: "Sisi kama
Watanzania, vijana wengi wameingia katika mkumbo wa kuiga vitu ambavyo
hawavijui." alisema na kusisitiza kuwa
vijana wanapaswa kutambua kuwa nguvu yao inapaswa kuelekezwa katika ubunifu na
uzalishaji, sio uharibifu.
Mwanasaikolojia wa Jamii Hussein maarifa akizungumza
kutoka Lindi anasema: "Kutokana na shinikizo la kijamii au kisiasa, vijana
wengi hujiingiza katika makundi ya vurugu. Tunahitaji kuimarisha elimu ya uraia
shuleni na vyuoni, kuwafanya vijana wajue wajibu wao kikatiba na kuona thamani
ya kuwa watulivu na wabunifu."
Aidha aliwataka vijana kugeuza mitandao yao kuwa
daraja la majadiliano chanya kuhusu ulinzi wa amani na usalama wa nchi kuliko
kusikiliza na kuiga na kufanya vurugu ambazo athari yake ni kubwa.

0 Maoni