Vitendo vya kuharibu miundombinu kama vile kuchoma
magari ya umma (BRT) vimekosolewa vikali, vikitajwa kama kukosa Uzalendo na
kujiharibia wenyewe. Uzalendo wa kweli una maana ya kuthamini na kulinda
rasilimali na miundombinu ya taifa, kwa kuwa ndiyo inayosaidia maisha ya
mamilioni.
Siraji Ali anahoji kwa uchungu: "Serikali
iliona kuna umuhimu wa kuleta magari mapya, leo hii yamechomwa moto sasa hii
inakuathiri mwenyewe; ulidai upewe kitu umepewa leo hii unakuja kukiunguza.
Sasa faida ni ya nani?" Anaongeza kuwa hata wafanyabiashara wakubwa
wameathirika kwa sababu "mzunguko wa kawaida wa maisha haukuwepo."
Faizat Peter alikumbusha kuwa "huo sio
utanzania," na kwamba lazima tujifunze yasitokee tena.
Aidha Siraji katika mahojiano alisema kwamba madhara
hayakuwa kwa Tanzania pekee bali hata nchi jirani ambazo zinategemea utulivu wa
Tanzania kupitisha mahitaji yao.
"Tanzania ni lango kuu la nchi jirani. Vurugu
hizi zimeathiri hata nchi jirani ambazo zinategemea Bandari yetu. Uzalendo ni
pia kutambua jukumu letu katika ukanda, na kuilinda amani yetu ni kulinda
uchumi wa nchi zingine."
Alisisitiza kuwa vitendo vya uharibifu vilivyofanywa
ni uhaini wa kiuchumi dhidi ya Watanzania na jirani zao.

0 Maoni