Baada
ya uchaguzi mkuu kufanyika na viongozi kuchaguliwa kihalali, Tanzania inajikuta
katika kipindi muhimu cha mtihani wa amani, utulivu, na upendo wa wananchi
wake. Huku jitihada za Serikali zikilenga uponyaji na maridhiano, wapo baadhi
ya watu wanaendeleza vitendo vya kuchochea vurugu kwa maslahi yao binafsi.
Kiongozi
Mkuu wa Nchi, Dk Samia Suluhu Hassan alipozindua Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, alitoa hotuba ya faraja iliyorejesha matumaini kwa Watanzania.
Hotuba hiyo ilibeba mwelekeo wa hatua za kuleta amani ya kudumu, ikiwemo:
akizungumzia uundwaji wa Tume ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vurugu
zilizotokea nchini;Kuangaliwa upya kwa mashtaka kwa wale waliokamatwa kutokana
na kusababisha vurugu, kwa lengo la kuwasamehe;Kuimarisha amani na mshikamano
kupitia mchakato wa maridhiano utakaosimamiwa na Kiongozi Mkuu na Kuanzisha
mchakato wa Katiba mpya kwa ajili ya mustakabali bora wa Taifa.
Hatua
hizi zimepokelewa kwa furaha kubwa na Watanzania wengi, ambao wanatamani
kurudisha utamaduni wa kuishi kwa amani na mshikamano ambao ndio asili yao.
Uhujumu
Amani kwa Maslahi ya Wafanyabiashara
Licha
ya jitihada hizi za kiserikali, kuna baadhi ya watu – ikiwemo wafanyabiashara
wanaoishi nje ya nchi – ambao wanaendeleza vitendo viovu vinavyolenga kuvuruga
amani yetu.
Watu
hawa wanadaiwa kuchochea vurugu na uharibifu wa mali za umma na binafsi kabla
na wakati wa uchaguzi, wakitumia kauli mbiu za uhamasishaji zilizopelekea maafa
yasiyosimulika kwa Watanzania.
Inaripotiwa
kuwa vurugu hizi zimekuwa 'biashara' inayowaingizia pesa wachache, huku
wakiungwa mkono na makundi ya kisiasa yanayotaka kupata madaraka kwa mgongo wa
mateso ya Watanzania kwa kukwepa kushiriki uchaguzi. Matendo yao maovu
yanaendelea kwa kueneza lugha za chuki na kuchochea vurugu mpya kwa tarehe
zijazo.
"Ndugu zangu Watanzania, tusikubali
kulishwa ujinga huu ambao ulipelekea majanga makubwa katika nchi jirani. Tangu
lini Watanzania tukawa na chuki za namna hii? Tuliendelee kulinda amani yetu.
Bila amani, hakuna elimu, hakuna biashara wala hakuna furaha."
Viongozi
wa Dini wanapaswa kuendelea kutumia nafasi zao kuwatoa wananchi kwenye mtanziko
huu wa kiusalama unaosababishwa na chuki zinazopandikizwa. Hakuna mshindi
katika 'mashindano' haya ya vurugu, bali Taifa zima linaoishi Tanzania ndilo
linapata hasara kwa kupoteza watoto, mali, na kuporomoka kwa uchumi.
Tanzania
ni Yetu Sote: Tusikubali kubomoa nchi yetu kwa uchochezi wa watu wasioishi
Tanzania. Kesho bora ya Tanzania itajengwa kwa kuendelea kuenzi amani,
kuvumiliana na kushirikiana.

0 Maoni