Sauti
ya wananchi nchini imekuwa wazi na yenye nguvu, ikituma ujumbe mmoja wa
kitaifa: Amani na Utulivu ndio msingi wa maendeleo. Baada ya matukio ya
kihistoria ya Oktoba 29, wananchi kutoka Tanga, Mbeya, Arusha, Dar es Salaam,
na mikoa mingine wamezungumza kwa uwazi kuhusu umuhimu wa kuijenga nchi kwa
maelewano, wakikataa vikali uchochezi unaoendelezwa kwa maslahi ya wachache.
Wananchi
katika maeneo mbalimbali wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hatari ya kuendeleza
ugomvi, wakisisitiza kuwa madhara ya vurugu yanawaathiri watu wa chini zaidi.
Wananchi
walionya kuwa Taifa limo mahali nyeti sana, ambapo chochezi ndogo inaweza
kuleta madhara makubwa kwa wajasiriamali wadogo kama mama ntilie, waendesha
bodaboda, na vijana wanaotafuta ajira.
Mbeya:
Waliuliza kwa uchungu, "Hivi tunayoyapigania kweli yanastahili kupoteza
maisha? Kupoteza mali? Kupoteza utulivu wa familia?" Walianza viongozi na
wananchi wote kutanguliza maridhiano na umoja mbele ya kila jambo la kisiasa.
Arusha:
Walisisitiza kuwa matukio ya Oktoba 29 yamefichua hatari ya vijana kutumiwa na
watu wenye maslahi binafsi. Walitoa wito kwa jamii kutotumia tena vijana kama
"nguvu kazi ya vurugu," bali kama washiriki muhimu wa kujenga uchumi
wa nchi.
Dar
es Salaam: Wananchi walisema taharuki ya siku zile imewafundisha kuwa chuki na
ushabiki usio na mwelekeo vina gharama kubwa. Walionyesha wazi kuwa
"Wanaochochea hawapo mtaani wakati sisi tunalia hasara."
Kwa
mujibu wa sauti hizi za umma, barabara za Tanzania hazihitaji "virusi vya
vurugu", bali zinahitaji kazi, utulivu, na fursa mpya za maendeleo.
Wananchi walionyesha imani yao kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua za
kulinda amani na kuhakikisha walioathiriwa na vurugu hizo wanasaidiwa kurejea
katika hali zao za kawaida.
Sauti
ya wananchi imeonyesha kuwa, licha ya uchungu uliopita, Watanzania wamejifunza
na wako tayari kulinda amani ya nchi kwa gharama yoyote.

0 Maoni