Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameshinda nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la 13 kwa kupata kura 348, huku mgombea mwenzake Steven Masele akiambulia 16 pekee.
Katika
uchaguzi huo nafasi ya Unaibu Spika ilitwaliwa na Mhe. Daniel Sillo aliyeibuka
kidedea baada ya kupata kura 362, huku wagombea wengine waliokuwa wamejitokeza
awali wakijitoa kabla ya upigaji kura kuanza.
Kwa uchaguzi
huo uliofanyika leo Jijini Dodoma sasa ni rasmi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania limepata viongozi wapya wa muhimili huo wa Serikali baada ya kufanyika
kwa uchaguzi wa Spika na Naibu Spika jijini Dodoma.
Katika Bunge
lililopita, Mhe. Mussa Azzan Zungu alikuwa Naibu Spika wa Bunge, huku Dkt.
Tulia Ackson ambaye alijitoa mapema kwenye mbio za kuwania Uspika alikuwa ni Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Taarifa kutoka
Bungeni zinaeleza kuwa jumla ya kura mbili (2) ziliharibika wakati wa mchakato
huo wa uchaguzi, ambao ulifanyika kwa uwazi na kufuata kanuni za Bunge

0 Maoni