Vurugu zilizotokea nchini hivi karibuni zimeacha
majeraha, lakini pia zimechochea wito wa kitaifa wa kurejea kwenye misingi ya
Utanzania Maadili Bora, Upendo, na Mashauriano katika kutatua migogoro.
Wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo walipohojiwa
walisisitiza kwamba vurugu si utamaduni wetu, na kwamba njia ya kutafuta haki
lazima iwe ya hekima, busara, na kuheshimu utu.
Siraji Ali Likwati, Mwenyekiti wa Bodaboda katika
maeneo ya Kimara Matangini, Michungwani, na King'ongo, anaeleza kwa msisitizo
mkubwa jinsi vurugu zinavyowaathiri hata wasiohusika.
"Kama
unataka haki basi haki fanya kwa namna haki inavyotakiwa kutakwa.
Kilichofanyika hapa kwetu sio kutaka haki kwa sababu unakuta duka la mangi hana
ushawishi wa siasa wa aina yoyote, yeye yupo na maisha yake anaendesha kwa
biashara zake, lakini watu wanakuja wanavunja, wanachukua mali zake. Hiyo
inakuwa mbaya zaidi."
Anasema kama wananchi wengine waliohojiwa
wanavyosema kwamba kuna namna ya kupeleka hoja lakini si kwa namna ya uporaji
na kupeleka maumivu kwa nina la kutafuta haki.
Pia, alisema kuna wajibu wa wananchi kusikiliza
viongozi waliokuwapo kwa mujibu wa katiba kwani hapakuwepo na sababu yoyote ya
msingi kuzuia tyukio la kikatiba kutekeleza tukio jingine la kikatiba kwa siku hiyo."Kiongozi akikwambia
fanyeni hivi, fanyeni alivyoagiza baadae mjadiliane." anasema Likwati
Wito huu unaungwa mkono na Viongozi wa Dini, ambao
wanasema Maadili Mema ndio nguzo ya jamii.
"Katika
Uislamu, tunafundishwa subira na kutafuta suluhu kwa njia ya amani na
mashauriano. Kuchukua mali ya mtu mwingine bila haki ni dhambi kubwa."
Kadhalika, pia kiongozi mmoja wa Kikristo anaongeza: "Biblia inatufundisha
upendo kwa jirani, na haki inapaswa kutafutwa kwa njia ya amani. Kufanya vurugu
ni kutengeneza makosa juu ya makosa."
Aidha, wataalamu wanahimiza matumizi ya Mashauriano na Upendo kama njia pekee ya kujenga taifa imara, huku tukiheshimu sheria na taratibu.

0 Maoni